Emerging Stars yatua nyumbani kutoka Tanzania

Emerging Stars watawaalika Ivory Coast katika duru ya kwanza ya raundi ya pili Novemba 9, kabla ya kuzuru Abidjan tarehe 17 mwezi ujao.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya ya soka kwa wanaume walio chini ya umri wa miaka 23, Emerging Stars, iliwasili  nyumbani jana Jumatano jioni kutoka Dar es Salaam nchini Tanzania.

Emerging Stars walijikatia tiketi kwa raundi ya pili kufuzu kwa fainali za bara Afrika (AFCON) mwaka ujao, kufuatia ushindi wa jumla wa mabao 5-4 dhidi ya Tanzania.

Kenya ilishinda mkondo wa kwanza mabao 4-1 uwanjani Nyayo kabla ya kushindwa na Tanzania 3-1 katika mechi ya marudio.

Emerging Stars watawaalika Ivory Coast katika duru ya kwanza ya raundi ya pili Novemba 9, kabla ya kuzuru Abidjan tarehe 17 mwezi ujao.

Mshindi wa mechi hiyo kwa jumla atafuzu kwa fainali za AFCON mwaka ujao nchini Misri, mashindano ambayo pia yatatumika kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2028.

Share This Article