Watu 8 wafariki kwenye ajali ya barabarani Tanzania

Ajali hiyo ilitokea alfajiri katika Kijiji cha lbihwa, Wilaya ya Bahi, wakati basi lililokuwa likisafiri kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam lilipogongana na basi lingine lililokuwa likielekea upande mwingine.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu wanane wafariki kwenye ajali ya barabarani Tanzania. Picha/Hisani.

Watu wanane wamefariki huku 66 wakijeruhiwa kwenye ajali ya barabarani iliyotokea Jumapili baada ya mabasi mawili ya abiria kugongana Jijini Dodoma Tanzania.

Ajali hiyo ilitokea alfajiri katika Kijiji cha lbihwa, Wilaya ya Bahi, wakati basi lililokuwa likisafiri kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam lilipogongana na basi lingine lililokuwa likielekea upande mwingine.

Akithibitisha ajali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, alisema waathiriwa saba walifariki papo hapo, huku mwingine akifariki kwa majeraha katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Kulingana na Senyamule, uchunguzi wa awali umebainisha kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya mmoja wa madereva kujaribu kupita gari lingine bila kuchukua tahadhari zinazohitajika.

Senyamule amesema manusura tisa wako katika hali mahututi, naye Afisa Mkuu wa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Ernest Ibenzi akidokeza kuwa manusura wanaendelea kupokea matibabu ya viwango tofauti katika hospitali hiyo.

TAGGED:
Share This Article