Arteta aongeza kandarasi ya miaka minne na Arsenal

Kandarasi hiyo mpya aliyosaini Mhispania huyo, inamfanya kuwa meneja anayelipwa donge nono katika Ligi Kuu Uingereza, akitarajiwa kulipwa pauni milioni 25 kwa mwaka.

Dismas Otuke
1 Min Read

Meneja wa mabingwa wa Uingereza Arsenal, Mikel Arteta, ameongeza kanadarasi mpya ya miaka minne ya kusalia kiwarani Emirates hadi Juni 30 mwaka 2030.

Arteta, aliyewaongoza The Gunners kutwaa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza msimu jana baada ya subira ya miaka 22, alishika hatamu za uongozi mwaka 2019.

Kandarasi hiyo mpya aliyosaini Mhispania huyo, inamfanya kuwa meneja anayelipwa donge nono katika Ligi Kuu Uingereza, akitarajiwa kulipwa pauni milioni 25 kwa mwaka.

Pia wasaidizi wake wote wamesaini mikataba mipya itakayodumu hadi mwaka 2030.

Share This Article