Ruto azindua rasmi jengo la kaburi la Hayati Raila

Uzinduzi huo ulifanyika huko Kang'o ka Jaramogi, Bondo, kaunti ya Siaya katika hafla iliyohudhuriwa na familia ya marehemu na viongozi kadhaa akiwemo Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi. 

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais William Ruto leo Jumatano amezindua rasmi jengo la kaburi la ukumbusho la Waziri Mkuu wa zamani Raila Amolo Odinga. 

Uzinduzi huo ulifanyika huko Kang’o ka Jaramogi, Bondo, kaunti ya Siaya katika hafla iliyohudhuriwa na familia ya marehemu na viongozi kadhaa akiwemo Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi.

Kisha Ruto aliweka shada la maua kwa kaburi la Raila ambaye kwa pamoja waliunda serikali jumuishi kabla ya mauti kumpata kinara huyo wa zamani wa chama cha ODM.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ruto alimlimbikizia Raila sifa sufufu akimtaja kuwa kiongozi aliyekuwa shupavu.

“‘Katika Raila Odinga, Kenya ilimpoteza kiongozi asiyekuwa wa kawaida. Kiongozi wa ujasiri usiokuwa wa kawaida, mwanamajumui wa Afrika na mzalendo aliyetoa maisha yake kupigania uhuru, haki na Kenya yenye utajiri ndani ya mipaka yake,” alisema kiongozi wa nchi.

Shughuli mbalimbali zimepangwa kufanyika kuanzia wiki ijayo kuelekea maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kutokea kwa kifo cha Raila wakati akipokea matibabu nchini India.

Raila alifariki Oktoba 15 mwaka jana.

 

 

Share This Article