Junior Starlets kupaa leo kwenda Uhispania

Kenya inayoshiriki Kombe la Dunia kwa mara ya pili na ya kwanza tangu mwaka 2024, imejumuishwa Kendi E,pamoja na Samoa,Uchina na Marekani katika kundi E.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya Kenya kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 17 -Junior Starlets, itaondoka nchini leo usiku kuelekea Uhispania kujiandaa kwa fainali za Kombe la Dunia.

Kikosi hicho ambacho kimekuwa kambini kwa takriban mwezi mmoja katuika uwanja wa Kasarani itakuwa Uhispania kwa wiki mbili kabla ya kuelekea Morocco kwa kipute cha Kombe la Dunia.

Kenya inayoshiriki Kombe la Dunia kwa mara ya pili na ya kwanza tangu mwaka 2024, imejumuishwa Kendi E,pamoja na Samoa,Uchina na Marekani katika kundi E.

Vipusa hao wanaofunzwa na Mildred Cheche wataanza kampeni yao dhidi ya Uchina tarehe 19 mwezi huu kabla ya kukabiliana  na Marekani siku tatu baadaye na hatimaye kufunga kazi dhidi ya Samoa Oktoba 25.

Share This Article