Rais William Ruto ameendelea na ziara yake katika Ukanda wa Pwani siku ya Alhamisi, siku moja baada ya kuzindua ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Lamu.
Awali, siku ya Jumanne, Ruto aliongoza uzinduzi wa kiwanda cha shilingi trilioni mbili cha kusafisha mafuta katika eneo la Lamu.
Baadhi ya miradi ya maendeleo iliyokaguliwa na Rais ni pamoja na ule wa uunganishaji umeme wa Iperanyi Mwandala, utoaji hatimiliki za ardhi eneo la Mwatate na ukaguzi wa ujenzi wa soko la Mwatunge, kaunti ya Taita Taveta.
Rais amekuwa katika Ukanda wa Pwani tangu mapema wiki hii.