Mfalme Mohammed wa sita amemteua Fatima Ezzahra kuwa Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke nchini Morocco kwa mujibu kwa ibara ya 47 ya katiba ya nchi hiyo .
Uteuzi huo ulitangazwa kufuatia mkutano ulioandaliwa kwenye Kasri ya Rabat na kuongozwa na Mfalme.
El Mansouri ambaye hadi uteuzi wake alikuwa mshirikishi wa shughuli za chama cha Authenticity and Modernity, kilichotwaa viti vingi katika uchaguzi wa mwezi jana,amekuwa mwanamke wa kwanza kupewa wadhifa huo mkuu Serikalini.
Katika hotuba yake ya kwanza El Mansouri alitaja uteuzi wake kuwa wa kihistoria akiahidi serikali itakayotimiza ndoto za raia wa Morocco na maono ya mfalme Mohammed wa sita.