Rais Ramaphosa atangaza operesheni dhidi ya mauaji ya wanawake

Agizo hilo linajiri huku sehemu kadhaa za taifa hilo zikighubikwa na visa vya mauaji ya wanawake, hasaa baada ya miili 12 ya wanawake kupatikana chini ya muda wa miezi miwili mashariki mwa Johannesburg.

Tom Mathinji
1 Min Read
Cyril Ramaphosa - Rais wa Afrika Kusini.

Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa, ametangaza operesheni kali ya kiusalama dhidi ya mauaji ya wanawake na ghasia za kijinsia.

Agizo hilo linajiri huku sehemu kadhaa za taifa hilo zikighubikwa na visa vya mauaji ya wanawake, hasaa baada ya miili 12 ya wanawake kupatikana chini ya muda wa miezi miwili mashariki mwa Johannesburg.

Ramaphosa alitangaza operesheni inayohusisha maafisa kutoka asasi mbalimbali za kiusalama kufuatia mauaji hayo, na watu 4 tayari wametiwa mbaroni.

Vifo hivyo vilisababisa lalama nyingi kuhusiana na kiwango cha dhulma dhidi ya wanawake nchini humo, hali hiyo ikitajwa kuwa dhulma baya zaidi dhidi ya wanawake kuwahi shuhudiwa ulimwenguni.

Huku akikiri kwamba serikali imezembea miaka ya hivi karibuni katika kukabiliana na dhulma za kijinsia, rais huyo alitangaza hatua kabambe kuanzia sasa zinazodhamiriwa kuwalinda watoto wasichana na wanawake.

Share This Article