Klabu ya Nairobi City Thunder inakaribia kukamilisha msimu wa tatu mtawalia wa ligi kuu ya mpira wa kikapu bila kushindwa baada ya kuilaza Kenya Ports Authority alama 2-0, katika mechi ya mchujo iliyochezwa katika ukumbi wa Makande kaunti Mombasa wiki iliyopita.
Thunder wameratibiwa kucheza mechi ya mwisho ya mchujo jijini Nairobi Oktoba mbili, ambapo wanatarajiwa kutawazwa mabingwa kwa msimu wa tatu kwa mpigo bila kupoteza mechi edapo watapata ushindi.
Klabu hiyo ambayo pia iliandikisha historia kuwa ya kwanza ya Kenya kushiriki Ligi mpira wa kikapu Afrika (BAL), inafadhiliwa na Benki ya I and M kwa kima cha shilingi milionio 10.