Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini, IEBC imeongeza orodha ya vituo ya kupigia kura kwa Wakenya wanaoishi ughaibuni kutoka 12 hadi 26.
Mwenyekiti wa IEBC, Erastus Ethekon, amesema hatua hiyo inalenga kuongeza idadi ya Wakenya wanaoishi ughaibuni watakaoshiriki uchaguzi mkuu mwakani.
Licha ya Wakenya milioni 1.46 kuishi ughaibuni, ni 62,000 pekee waliopiga kura katika uchaguzi mkuu uliopita.
Vituo vipya vya kupigia kura kwa Wakenya walio ughaiubuni vitawekwa katika nchi zinazojumuisha Saudi Arabia, Botswana, Oman, Australia, Uswidi, Uswizi, Uholanzi na Ghana.
Nchi zingine ni Italia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Nigeria, Ireland, Uturuki, Ethiopia, China, Msumbiji, Afrika Kusini, Canada, Uingereza na Marekani.
Aidha, IEBC imesema inalenga kuwasajili Wakenya milioni 1.8 kwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, ingawa inakabiliwa na nakisi ya bajeti, ikiwa na shilingi milioni 400 pekee kati ya shilingi milioni 502 zinazohitajika.
Uchaguzi mkuu wa mwaka ujao utaandaliwa Agosti 10.