Timu ya Kenya iliyotwaa ubingwa wa dunia wa mbio za barabara nchini Denmark inatarajiwa kurejea nchini mapema Jumanne.
Kenya iliyowajumuisha wanariadha 16 ilishinda dhahabu 3 fedha 3 na shaba moja .
Bingwa wa dunia wa mbio za nyika Agnes Jebet Ngetich alinyakua dahahabu na kuweka rekodi mpya ya dunia ya dakika 65 sekunde 5 nukta 16.
Timu ya Kenya itawasili nchini mapema Jumanne kwa kutumia ndege ya Emirates nambari ya usajili EK 717.