Rais William Ruto amesema mpango wa nyumba za gharama nafuu, umebadilisha na kupandisha hadhi ya Wakenya wengi wa kipato cha chini hususan wanaoishi kwenye mitaa duni.
Akizungumza katika mahojiano ya moja kwa moja na wanahabari kutoka Ikulu ndogo ya Kisumu, Rais alisema nyumba hizo zilizo katika vitengo vitatu kulingana na kipato cha kila mmoja, zitasaidia kumaliza tatizo la ongezeko la mitaaa ya mabanda.
Aidha, Rais alidokeza kuwa nyumba hizo pia zimetoa ajira kwa idadi kubwa ya Wakenya.
Alifafanua kuwa hazina ya nyumba pia imesaidia miradi mingine ya serikali kama ujenzi wa masoko ya kisasa.
Rais Ruto yuko kwenye ziara rasmi katika eneo la Nyanza.