Mshindi wa nishani ya fedha ya Dunia Dorcas Ewoi wa Kenya,atatimka fainali ya mita 1,500 Jumamosi usiku katika siku ya opili ya makala ya kwanza ya mashindano ya Ultimate mjini Budapest,Hungary.
Ewoi anayeorodheshwa wa pili katika msimamo wa Dunia atakabiliana na Jessica Hul wa Australia anayeshikilia nafasi ya kwanza ulimwenguni ,Georgia Hunter Bell wa Uingereza aliye wa tatu,na Birke Haylom wao Ethiopia anayeshikilia nafasi ya nne.
Fainali hiyo itaanza saa mbili na dakika 36 usiku.
Aidha,bingwa wa Dunia na Olimpiki Emmanuel Wanyonyi atatimka nusu fainali ya mita 800.