Kivumbi chatarajiwa FKF ikiandaa AGM leo

Wanachama hao saba wa kamati kuu yamkini pia  wanalalamikia kutohusishwa au kushauriwa katika maamuzi muhimu yanayohusu shirikisho.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kivumbi kinatarajiwa huku Shirikisho la Soka nchini Kenya, FKF likitarajiwa kuandaa mkutano mkuu wa mwaka (AGM) leo Alhamisi, Septemba 10.

Kumekuwa na msukosuko ndani ya Baraza Kuu la FKF (NEC) huku ikidaiwa kuwa wanachama saba walikuwa wanapinga baadhi ya ajenda katika kikao hicho cha leo.

Wanachama hao saba wa kamati kuu yamkini pia  wanalalamikia kutohusishwa au kushauriwa katika maamuzi muhimu yanayohusu shirikisho.

Kikao hicho kinaandaliwa wakati pia kungali na tandabelua kuhusu kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya wanaume ambayo tayari imecheleweshwa kwa majuma mawili.

Siku ya Jumatano, Waziri wa Michezo Salim Mvurya alikutana na wenyeviti wa vilabu vyote vinanvyoshiriki ligi hiyo akiwataka kutatua tofauti zao ili kuruhusu kuanza kwa ligi.

Share This Article