Ruto amaliza ukiritimba wa kampuni ya TATA Chemicals

Kampuni ya Tata Chemicals ilianza kuchimba madini ya magadi mwaka 1911 nchini Kenya.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ametangaza upya zabuni ya uchimbaji madini ya magadi katika kaunti ya Kajiado na kukomesha ukiritimba wa kambuni ya TATA Chemicals, ambayo imekuwa ikiendesha bishahara hiyo kwa kipindi kirefu nchini Kneya.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kisiasa katika eneo hilo ,Ruto alisema kuwa kampuni kadhaa zitatuma maombi ya zabuni hiyo huku kampuni zaidi ya moja zikipewa tenda kinyume na ilivyo kwa sasa.

Aidha,Ruto alisema kamwe hatakubali kampuni yoyote itakayochimba madini hayo kumiliki zaidi ya asilimia 30 ya ardhi ya Kajiado.

Madini ya magadi hutumiwa kutengeza  glasi,kemikali za kutengeza sabuni ,pamoja na kutengeza chumvi ya mifugo na binadamu.

Rais alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikiwapunja wakenya katika sehemu hiyo huku madini hayo yakikosa kuwafaidi wakazi.

Kampuni ya Tata Chemicals ilianza kuchimba madini ya magadi mwaka 1911 nchini Kenya.

Mapema wiki hii Ruto pia alitangaza kuwa asilimia 70 ya ardhi inayomilikiwa na kampuni hiyo kupitia kwa ukodishaji itarejeshewa wenyeji wa eneo hilo.

 

Share This Article