Pirikapirika za kuwaokoa manusura zaendelea nchini Nepal

Mamlaka nchini Nepal zinasema watu 1,259 wamefariki tangu kutokea kwa mafuriko ya ghafla Agosti 26 huku wengine zaidi ya 5,000 wakiwa hawajulikani walipo.

Martin Mwanje
1 Min Read
Utafutaji wa manusura ukiendelea kufuatia mafuriko ya ghafla nchini Nepal / Picha kwa hisani ya France 24

Timu za uokoaji nchini Nepal zimo mbioni kutafuta manusura zaidi wa mafuriko makubwa ya ghafla yaliyotokea nchini humo Agosti 26 mwaka huu. 

Mafuriko hayo yalitokea kwenye eneo la mpaka na China.

Timu hizo zimeimarisha jitihada za kuwatafuta wafanyakazi watu waliokwama ndani ya mitambo ya umeme huku ripoti zikiashiria  yamkini baadhi yao bado wako hai.

Mamlaka nchini Nepal zinasema watu 1,259 wamefariki tangu kutokea kwa mkasa huo huku wengine zaidi ya 5,000 wakiwa hawajulikani walipo.

Ripoti za vyombo vya habari nchini China zinaashiria watu 21 wamefariki kutokana na janga hilo nchini humo huku wengine zaidi ya 540 wakiwa hawajulikani walipo.

Ripoti zinaashiria takriban watu 900 wamekwama katika mitambo mbalimbali ya umeme.

 

Share This Article