Nyumba 1,000 huenda zikumbwe na mafuriko Nairobi

Kulingana na idara ya Utabiri wa hali ya hewa nchini nyumba hizo zilizo katika maeneo yapatayo 246 huenda zikaathiriwa na mafuriko.

Dismas Otuke
1 Min Read

Takriban nyumba 1,000 huenda zikaathiriwa na mafuriko ambayo huenda  yakaletwa na mvua kubwa ya El Nino, inayotarajiwa kuanza baadaye mwezi ujao hadi Disemba.

Kulingana na idara ya Utabiri wa hali ya hewa nchini nyumba hizo zilizo katika maeneo yapatayo 246 huenda zikaathiriwa na mafuriko.

Idara hiyo imesema kuwa maeneo mengi humu nchini huenda yakashuhudia mvua za kadri na kiwango cha juu katika kipindi hicho na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari.

Maeneo hayo ni kama vile Uhuru Highway,Jogoo Road,Kangundo Road na Thika Road.

Mitaa inayotarajiwa kukumbwa na mafuriko ni Industrial Area,Pipeline,Kware na Imara Daima.

Pia katikati ya ya jiji la Nairobi inatarajiwakuathiriwa na mafuriko .

 

 

 

 

TAGGED:
Share This Article