Bingwa wa Dunia na Olimpiki Peres Jepchirchir wa Kenya, ametwaa ubingwa wa mbio za Sydney Marathon zilizoandaliwa mapema Jumapili nchini Australia.
Jepchirchir ametwala mbio hizo akikata utepe kwa muda wa saa 2 dakika 18 na sekunde 31, na kunyakua taji ya nne ya mbio kuu za marathon Duniani.
Irene Cheptai pia wa Kenya amemaliza wa pili kwa saa 2 dakika 22 na sekunde 11, huku Shure Dimise wa Ethiopia, akiridhia nafasi ya tatu.
Mkenya mwingine Priscah Cherono alimaliza wa sita .
Ethiopia pia ilitwaa nafasi mbili za kwanza katika mbio za wanaume,Adissu Gobena, akiibuka mshindi kwa saa 2 dakika 4 na sekunde 42,akifuatwa na Chimdessa Gudeta sekunde 3 baadaye.
Ramakongoana Tebello kutoka Botswana, alimaliza wa tatu huku Vincent Ngetich wa Kenya akichukua nafasi ya saba.