Wizara ya afya iko tayari kukabiliana na magonjwa yatokanayo na mafuriko

Katibu katika wizara ya afya Mary Muthoni amesema serikali iko tayari kukabiliana na magonjwa kama vile kipindundu,homa ya matumbo,kichocho na homa ya ini na magonjwa mengine ya kuendesha ambayo husambaa sana wakati wa mvua.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wizara Afya imetangaza kuwa iko tayari kukabiliana na magonjwa yanayotokana na mafuriko huku mvua kubwa ikitirajiwa nchini kuanzia mwezi Septemba.

Kwenye taraifa kwa umma wizara ya afya imesema imebuni jopo linalojumuisha sekta mbalimbali ili kupunguza magonjwa na vifo vinavyohusiana na maji ya mafuriko na mvua kubwa.

Katibu katika wizara ya afya Mary Muthoni amesema serikali iko tayari kukabiliana na magonjwa kama vile kipindundu,homa ya matumbo,kichocho na homa ya ini na magonjwa mengine ya kuendesha ambayo husambaa sana wakati wa mvua.

Wizara ya afya imewataka wakenya kuchukua tahadhari ifaayo kama vile kuzingatia usafi wa maji na vyakula na kutafuta matibabu mapema.

Mikakati iliyowekwa na serikali ni pamoja na:-kutenga maabara ya uchunguzi,kuweka tayari dawa za matibabu na kuandaa jamii kwa mkurupuko wowote kupitia kwa wastawishaji afya ya jamii.

TAGGED:
Share This Article