Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ilianza kuwachanja raia wake dhidi ya ugonjwa wa Ebola siku ya Alhamisi katika juhudi za kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya Bundibugyo.
Kulingana na Waziri wa Afya nchini Congo,Samuel Kamba wamepokea dozi 50,000 za chanjo aina ya Everbo kutoka kwa shirika la Afya Ulimwenguni(WHO) ili kupambana na maambukizi ya Ebola.
Chanjo hiyo ilianza kutolewa kwa raia wa eneo la Kisangani,mji mkuu wa mkoa wa Tshopo.
Mkoa wa Kisangani ni mojawapo wa mikoa sita yenye maambukizi makubwa ya Ebola.
DRC imeripoti visa vya maambukizi ya Ebola 5,794 na jumla ya vivo 2,786 tangu kutangazwa kuzuka kwa ugonjwa huo Mei 15 mwaka huu.