Samia afanya mageuzi ya Wakuu wa Mikoa,awateua wanne wapya

Kwenye mabadiliko hayo Rais Samia aliwahamisha Wakuu wa mikoa sita.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Tanzania siku ya Alhamisi alifanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa huku akiwateua wengine wanne wapya waliokuwa wameanguka uchaguzi kwa tiketi ya chama cha CCM.

Kwenye mabadiliko hayo Rais Samia aliwahamisha Wakuu wa mikoa sita.

Mbunge wa zamani wa Misungwi ,Alexander Mnyeti aliteuliwa Mkuu mpya wa mkoa wa Geita naye mbunge wa zamani wa Maswa Mashariki Stanlaus Nyongo, akiteuliwa Mkuu wa mkoa Pwani.

 

Share This Article