Mkuu wa majeshi nchini Uganda Muhoozi Kainerugaba ambaye ni mwanawe Rais Yoweri Museveni ametangaza kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2031.
Akijigamba kupitia ukurusa wake wa X, Muhoozi amesema ana uhakika wa kupata asilimia 90 ya kura akiungwa mkono na babake.
Hatua hiyo inathibitisha uvumi ambao umekuwa ukizagaa kuhusu uwezekano wa Muhoozi kumrithi babake.
Awali, alikisiwa kuwania kiti hicho kwenye uchaguzi wa mapema mwaka huu lakini akajiondoa.