Wenyeji Kenya waikomoa Zambia, Voliboli ya vipusa Afrika

Pambano hilo lililosakatwa katika ukumbi wa Kasarani, lilishuhudia Kenya wakipata ushindi  kirahisi wa seti za 25-14, 25-9 na 25-11, wakimaliza mchezo kwa pointi 75 kwa 34.

Dismas Otuke
1 Min Read

Malkia Strikers ya Kenya walianza vyema kampeni ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vipusa, walipowazabua Zambia seti 3-0 katika mechi yao ya ufunguzi ya kundi A Jumanne usiku.

Pambano hilo lililosakatwa katika ukumbi wa Kasarani, lilishuhudia Kenya wakipata ushindi  kirahisi wa seti za 25-14, 25-9 na 25-11, wakimaliza mchezo kwa pointi 75 kwa 34.

Kocha wa Kenya Geoffrey Omondi alifurahia matokeo hayo akisema, “Tunafurahia kuanza mashindano kwa ushindi licha ya kupata ushindani mkali. Tunajipanga kujiandaa vyema kwa mchuano wa Mali, tunawaomba mashabiki kuja kwa wingi kutushabikia. Tunaelewa umuhimu wa mashindano hayana tutajituma kuhakikisha tuanapata ubingwa.”

Mashindano hayo yanashirikisha mataifa 15 huku yakiandaliwa katika viwanja vya Kasarani na Ulinzi.

Yatakamilika Septemba 5 ambapo mshindi atawakilisha bara kwa mashindano ya Dunia mwaka ujao.

Share This Article