Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Voliboli ya Wanawake yataingia siku ya pili Jumatano huku jumla ya mechi saba zikichezwa katika viwanja vya Kasarani na Ulinzi Complex.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC itakabiliana na Rwanda katika uwanja wa Kasarani kaunzia saa nne, kabla ya Uganda kumenyana na Burkina Faso saa tano katika ukumbi wa Ulinzi.
Algeria watakabana koo na Burundi saa saba katika uwanja wa Kasarani, nao Zambia wachuane na Mali saa nane katika uwanja wa Ulinzi.
Saa kumi alasiri, itakuwa zamu ya Misri kutoana jasho na Senegal katika uwanja wa Kasarani, nao Nigeria washuke uwanjani Ulinzi dhidi ya Ghana saa kumi na moja.
Cameroon watafunga ratiba ya siku kwa kumenyana na Tunisia kuanzia saa moja usiku katika uchanjaa wa Kasarani.