Mabingwa wa Kenya Gor Mahia wameratibiwa kuchuana na miamba wa Misri Pyramids katika mkumbo wa kwanza wa awamu ya mchujo kuwania kombe la ligi ya Mabingwa Afrika.
Duru ya kwanza itasakatwa Septemba 6 katika uwanja wa Nyayo, kabla ya mechi ya marudio kuchezwa Septemba 13 jijini Cairo.
Pyramids walishinda ubingwa wa Afrika kwa mara ya kwanza mwaka 2025, wanatarajiwa kuwasili Nairobi tarehe 3 mwezi ujao.