Ni afueni kwa wakulima baada ya Rais William Ruto kutangaza kuwa mbolea ya mfuko wa kilo 50 itauzwa kwa shilingi 2,000.
Awali, mbolea hiyo iliuzwa kwa shilingi 2,500.
Ruto amesema bei hiyo mpya itaanza kutekelezwa ndani ya kipindi cha majuma mawili yajayo.
Akizungumza huko Taita Taveta, Rais amewataka wakulima kutumia fursa hiyo kuboresha kilimo chao msimu ujao wa upanzi.
Aidha, Rais alitangaza kuwa serikali itapunguza bei ya mbegu ya mahindi kwa asilimi 50.
Mbolea ya ruzuku imekuwa ikiuzwa kwa shilingi 2,500 tangu mwanzo wa utawala wa Rais Ruto kutoka bei ya awali ya shilingi 5,000.