Wauguzi waapa kuendelea na mgomo

Chama hicho kimesema kuwa serikali imepuuzilia mbali matakwa yao na kufeli kusaini mwafaka wa kurejea kazini wa mwaka 2017 waliokuwa wameafikiana.

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha kitaifa cha wauguzi nchini(KNUN) kimeapa kuendelea na mgomo wake wa kitaifa na kulemaza utoaji huduma za afya katika hospitali za umma kote nchini.

Chama hicho kimesema kuwa serikali imepuuzilia mbali matakwa yao na kufeli kusaini mwafaka wa kurejea kazini wa mwaka 2017 waliokuwa wameafikiana.

Katibu Mkuu wa KNUN Seth Panyako amesema kuwa watapuuza agizo la mahakam lililowataka kufutilia mbali mgomo likiuharamisha.

Aidha,Panyako ameshutumu baraza la Magavana nchini alilotaja kuwa linahujumu juhudi zao kwa kushirikiana na tume ya kuratibu mishahara ya wafanyakazi wa umma (SRC).

Mgomo huo unaoendelea ulisababisha hospitali kuu ya Kenyatta ilitoa arifa kwa wagonjwa wanaotafuta huduma zisizo za dharura kutafuta matibabu kwenye vituo vingine kutokana na mgomo huo wa wauguzi.

Share This Article