Mabingwa wa Ligi kuu Kenya Gor Mahia FC na mabingw wa Kombe la Mozzart watashuka dimbani Nyayo siku ya Jumapili Agosti 23, kuwania kombe la Super ambalo ni fungua pazia ya msimu mpya wa Ligi.
Timu zote pia zinajiandaa kwa majukumu yaliyo mbele yao ya kuiwakilisha Kenya katika ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho mtawalia.
Msimu mpya wa Ligi Kuu Kenya umeratibiwa kung’oa nanga juma lijalo.

Gor walitawazwa mabingwa wa Ligi ya Kenya kwa mara ya 22 msimu jana walipozoa alama 69 nao Tusker wakaambulia nafasi ya tisa kwa pointi 45.