Serikali ya Tanzania imetoa msaada wa vifaa vya matibabu vya thamani ya shilingi milioni 22 sawa na milioni moja ya Kenya kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.
Msaada huo ulijiri wakai ambapo Rais wa DRC Felix Tshishekedi alipozuru Tanzania kwa ziara rasmi ya siku mbili.
Kulingana na waziri wa Afya wa Tanzania Mohammed Mchengerwa msaada huo utapiha jeki juhudi za DRC kukabiliana na maambukizi ya Ebola.
DRC inatarajiwa pia kupokea dozi za chanjo Everbo kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kusaidia kukabiliana na maambukizi mapya ya Ebola.