Bingwa wa Dunia na Olimpiki katika mbio za mita 800 Emmanuel Wanyonyi atawaongoza Wakenya Alhamisi usiku katika mashindano ya Laussane Diamond League nchini Uswizi, akilenga kudumisha uongozi wake.
Wanyonyi aanyeongoza msimamo Kwa alama 27, atakabiliana na Marco Arop wa Canada,Djamel Sedjati wa Algeria,Brandon Miller wa Marekani na Gabriel Tual wa Ufaransa.
Bingwa wa Dunia Kwa wanawake Lillian Odira, atajitosa uwanjani akilenga kuboresha nafasi yake ya 8 anayoshikilia akiwan na alama 14.
Odira aneyewinda ushindi wa pili atakabiliana na Audrey Werro wa Uswizi, anayeongoza msimamo,Prudence Sedgodisso wa Afrika Kusini na Willey Adson wa Marekani miongoni mwa wengine.
Bingwa wa Olimpiki Faith Cherotich, anayeshikilia nafasi ya pili atakabiliana na Marwa Bouzayani wa Tunisia, anayeongoza msimamo pamoja na mtani wake wa jadi Winfred Yavi Wa Bahrain kwenye fainali ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji.