Watu zaidi ya laki mbili watoroka makwao huko Kordofan nchini Sudan

Katika eneo la Blue Nile, watu wapatao 78,000 wamekimbia makwao huku 18,000 wakitoroka eneo la magharibi mwa Darfur katika nusu ya kwanza ya mwezi huu wa Agosti.

Dismas Otuke
1 Min Read

Watu zaidi ya laki mbili wamefurushwa makwao katika eneo la Kordofan nchini Sudan kutokana na mapigano yaliyozuka mwaka jana.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, UN vita ambavyo vimekuwa vikiendelea tangu mwaka jana kupitia kwa droni na mashambulizi ya angani vimeathiri miundombinu muhimu ikiwemo umeme na maji katika mji wa El Obeid.

UN imeongeza kuwa mafuriko yaliyoshudiwa katika eneo hilo lililo karibu na Darfur Kaskazini yamefanya hali kuwa tete zaidi.

Aidha, mapigano makali ambayo yameshuhudiwa eneo la El Obeid pia yamesababisha kutoweka kwa umeme na kukatizwa kwa maji, misongamao mikubwa hospitalini na hata kukatiza mawasiliano ya simu.

Katika eneo la Blue Nile, watu wapatao 78,000 wamekimbia makwao huku 18,000 wakitoroka eneo la magharibi mwa Darfur katika nusu ya kwanza ya mwezi huu wa Agosti.

Wakati hou huo, mvua kubwa iliyonyesha kaskazini mwa Darfur na eneo la Tawila imeharibu nyumba zipatazo 1,350 huku familia zaidi ya 1,000 zikiachwa bila makao.

Share This Article