Shirikisho la kandanda nchini Nigeria limemtimua kocha wat imu ya taifa ya wanawake Super Falcons, Justine Madugu na benchi lote la kiufundi, kufuatia matokeo dunia baada ya miamba hao kukosa kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao kwa mara ya kwanza.
Madugu alishika hatamu za kuinoa Nigeria mwaka 2024, na kuwawesha kunyakua Kombe la Afrika kwa mara ya 10 mwaka jana.
Hata hivyo kukosa kufuzu kwa nusu fainali katika mashindano ya WAFCON mwaka huu nchini Morocco, kumeiponza Super Falcons ambao sasa watakosa kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1991.
Shirikisho la Nigderia,NFF limeanza uchunguzi kubaini kiini cha matokeo hayo mabovu huku Rais Ibrahim Gusau, akibuni jopokazi la kutathmini kilichotokea.