Meneja wa Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru nchini Uganda(URA) amekamatwa jijini Kampala, Uganda baada ya kufumaniwa akipokea hongo ya dola 60,000 za Kimarekani sawia na shilingi milioni 7.7 za Kenya.
Inadaiwa Geoffrey Ssozi ambaye ni Meneja wa Masuala ya Nje katika Forodha ya Uganda alitaka apewe rushwa ya dola laki moja kutoka kwa mwekezaji wa kibinafsi wa kigeni ili kumkinga dhidi ya uchunguzi wa akaunti za fedha uliokuwa ukitekelezwa katika kampuni yake.
Ssozi alifumaniwa katika hoteli moja jijini Kampala akipokea hongo hiyo Alhamisi wiki jana na kukamatwa kwa kosa la kula mlungula.
Maafisa wa polisi walidokezwa kuhusu dili hiyo na mtu mmoja na kuweka mtego ndiposa wakawanasa Ssozi pamoja na afisa aliyepiga dili hiyo.