Walioangamia kwa mkasa wa feri Zimbabwe wafikia 80

Feri hiyo inayomilikiwa na serikali ilipinduka juu chini Jumanne wiki jana kutoka na idadi kubwa ya wasafiri.

Dismas Otuke
1 Min Read

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mkasa wa kuzama kwa feri nchini Zimbabwe imefikia 80.

Hii ni baada ya miili zaidi kupatikana jana Jumapili.

Feri hiyo inayomilikiwa na serikali ilipinduka juu chini Jumanne wiki jana kutoka na idadi kubwa ya wasafiri. Yamkini ilikuwa imebeba watu 114, waendeshaji watano na idadi isiyojulikana ya watoto.

Kwa kawaida, feri hiyo inamudu idadi ya watu 90 pekee.

Iliripotiwa kuwa watu 77 waliokolewa katika ajali hiyo Ziwani Kariba, takriban kilomita 400 magharibi mwa mji mkuu wa Harare.

Manusura walisema kuwa walijaribu kumwomba nahodha wa feri hiyo arudi nyuma kutokana na mawimbi makali baada ya kuona kuwa ilikuwa imeanza kuingia maji kutoka mwanzoni mwa safari, ila akakaidi.

Share This Article