Washukiwa wawili wa wizi wa lori la usafirishaji mizigo wamekamatwa na maafisa wa polisi wa kituo cha Andungosi eneo la Teso Kusini.
Kulingana na taarifa kutoka kwa idara ya DCI,wanaume hao wawili walikamatwa na lori aina ya Isuzu lililoripotiwa kuibwa mjini Naivasha Agosti 16.
Polisi waliokuwa wakliendesha msako barabarani katika eneo la Andungosi barabara ya Buteba, walifumania lori hilo lenye nambari za usajili KAR 906Z, na kuwakamata dereva ambaye ni raia wa Uganda,Ayo Haruna na mshirika wake Abdalla Kipserem.


Wawili hao wako korokoroni huku polisi wakiendesha uchunguzi .