Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan, amesema Misri huenda ikajiunga na mkataba wa pamoja wa ulinzi uliotiwa saini hivi karibuni na Uturuki, Saudi Arabia na Pakistan.
Kulingana naye hatua hiyo inaweza kusababisha mkataba huo kupata wanachama zaidi.
Akizungumza kwenye mahijiano na Al Jazeera Erdoğan alisema Makubaliano ya Pamoja ya Ulinzi ya Mecca yanawataka waliotia saini kuchukua hatua za pamoja iwapo mmoja wao atashambuliwa kutoka nje.
“Makubaliano haya yametuma ujumbe muhimu kwa dunia,” Erdoğan alisema, akiongeza kuwa ushiriki wa Misri ni miongoni mwa chaguo zinazozingatiwa kwa ajili ya kupanua makubaliano hayo siku zijazo.
Mkataba huo, unaojulikana pia kama Mkataba wa Mecca, ulitiwa saini katika mji mtakatifu Ijumaa iliyopita na Erdoğan, Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman na Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif.
Unasema kwamba shambulio la kijeshi dhidi ya mmoja kati ya nchi hizo tatu litachukuliwa kuwa shambulio dhidi yao wote.
Wadadisi wanafananisha kifungu hicho cha kuzuia mashambulizi kwa pamoja na kifungu nambari 5 cha mkataba wa NATO.
Erdoğan alizungumza kuhusu masuala mbalimbali ya kikanda, yakiwemo mvutano kuhusu Mlango-Bahari wa Hormuz pamoja na vita nchini Syria, Gaza na Lebanon.
Kiongozi huyo wa Uturuki alisema kufunguliwa tena kwa mlango huo ni kipaumbele kwa Ankara, akisema kuendelea kuufungwa hakumsaidii yeyote.
Alisifu Qatar kwa kutekeleza jukumu muhimu katika juhudi za upatanishi zinazolenga kusitisha mapigano katika eneo hilo, akiahidi kuwa Uturuki haitawaacha majirani zake wakabiliane na machafuko ya kikanda peke yao, akitaja Syria, Gaza na Lebanon.
Alisema Ankara itafanya kila iwezalo kuunga mkono utulivu nchini Syria, huku akitaja mipango yake ya…