Mwanamuziki wa Kenya Nyota Ndogo amesiulia kile anachokitaja kuwa kitu cha ajabu kilichomtokea kwenye hafla ya Usiku wa Lulu ya Jamii.
Kupitia video aliyonakili na kuchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Nyota anasema punde baada ya kuondoka jukwaani kutumbuiza kwenye hafla hiyo, mama mmoja alimfuata na kumwambia kwamba yeye amerogwa.
Mama huyo alimdadisi Nyota asiamini kwamba ni yeye, lakini alipomhakikishia, alisisitiza kwamba amerogwa na kwamba yeye na familia yake wamekuwa wakimfuatilia na kumsema kuhusu kazi yake.
Hakumpa maelezo zaidi kuhusu aliyemroga lakini alimwelekeza kwamba awe akisali mara kwa mara na kutafuta walimu wa dini mara tatu kwa wiki wamsemee dua.
Msanii huyo hata hivyo alisema kwamba hataki kuamini maneno ya mama huyo wala kuamini uchawi upo. “Ninaamini kwamba Mwenyezi Mungu yupo na Mwenyezi Mungu ananilinda na ataendelea kunilinda na familia yangu,” alijitia moyo msanii huyo.
Kulingana naye, kila msanii ana muda wa kuwa nyota na kupata pesa nyingi kutokana na usanii na muda huo hufika mwisho akitoa mfano wa wasanii waliomtangulia waliofanya vizuri kabla yake kuja na anaamini kizazi kingine cha wasanii kitakuja baada yake.
Mwimbaji huyo alizungumzia kazi ambazo amepata mfululizo katika siku za hivi maajuzi akisema zimeletwa na Mungu na alishangaa kwamba mashabiki bado wanakumbuka nyimbo zake na walikuwa wakiimba naye.