Polisi wanasa mifugo 470 waliokuwa wameibwa Marsabit

Kikosi hicho kiliwaandama majangili waliotekeleza wizi huo, ambapo walishindwa nguvu na kuwaacha mifugo hao 470, kabla ya kutorokea katika milima ya Ruai.

Tom Mathinji
1 Min Read
Polisi wapata mifugo 470 waliokuwa wameibwa Marsabit.

Maafisa wa asasi mbali mbali za usalama, wamefanikiwa kupata mifugo 470 waliokuwa wameibwa katika eneo la Galgumbe, Loiyangalani, kaunti ya Marsabit.

Kikosi hicho kiliwaandama majangili waliotekeleza wizi huo,ambapo walishindwa nguvu na kuwaacha mifugo hao 470, kabla ya kutorokea katika milima ya Ruai.

Huduma ya Taifa ya Polisi (NPS), kupitia ukurasa wa X, imesema operesheni za kiusalama zimeimarishwa katika eneo hilo ili kuwatafuta na kuwakamata wahalifu, kurejesha utulivu na kuwatafuta mifugo ambao wameibwa.

“Huduma ya Taifa ya Polisi inawapongeza maafisa wa asasi mbalimbali za usalama kwa kuchukua hatua za haraka zilizofanikisha kupatikana kwa mifugo hao,” ilisema NPS kwenye taarifa.

Huduma hiyo ilitoa wito kwa umma kuripoti shughuli zinazotiliwa shaka katika kituo cha polisi kilicho karibu.

Share This Article