Chepkwech anyakua dhahabu ya mita 1500

Dismas Otuke
1 Min Read
Wilson Chepkwech akikamilisha mbio za mita 1500.Picha hisani:Aaron Bui

Wilson Chepkwech alinyakua nishani ya dhahabu ya mbio za mita 1500 huku David Kapaiko akishinda fredha katika siku ya mwisho ya mashindano ya Riadha Duniani kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 yaliyokamilika Jumapili jioni katika jimbo la Oregon nchini Marekani.

Chepkwech aliziparakasa mbio hizo kwa dakika 3 sekunde 37.46, huku Kapaiko akishinda fedha kwa dakika 3 sekunde 38.32 ,naye Ousama El Redouni wa Morocco, akaambulia shaba

Kenya pia ilishinda fedha na shaba katika fainali ya mita 3,oo0 kuruka maji na viunzi  kupitia kwa Emmanuel Lemiso na  na Nicholas Losiwareng mtawalia.

Dhahabu ilitwaliwa na Bakr El Asri wa Uhispania.

Share This Article