Josephine Sembeyo Mancha alinyakua nishani ya dhahabu huku Caren Chepchir Serem akinyakua shaba katika fainali hya mbio za mita 1500, katika siku ya mwisho ya mashindano ya Riadha Duniani kwa chipukizi walio chini ya umri wa m,iakla 20 Jumapili usiku mjini Oregon,Marekani.
Macha aliye na umri wa miaka 19 alihitaji kujizatati katika mita 150 za mwisho na kunusu dhahabu akizikamilisha kwa mud awa dakika 4 sekunde 16.73,sekunde 0.04, nyuma ya Mmarekani Clair Stegall, aliyeshinda fedha huku Chepchirchir akiridhia shaba.

Kenya ilimaliza ya pili kwenye jedwali la nishani kwa dhahabu 4 fedha 3 na shaba 4,nyuma ya wenyeji marekani waliotwaa ubingwa kwa dhahabu 12,fedha 7 na shaba 5.
Mashindano hayo ya siku nne yaliwaleta Pamoja zaidi ya wanariadha 1,800 kutoka mataifa 147.