Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi, amesema umoja wa nchi ni nguzo kuu kwa maendeleo ya kudumu katika taifa la Kenya.
Mudavadi alidokeza kuwa, huku taifa linapojiandaa kwa Uchaguzi Mkuu mwaka 2027, Wakenya wanapaswa kukataa migawanyiko na kukumbatia umoja na ufanisi wa pamoja.
“Ni kwa msingi huu ndiposa utawala wa Kenya Kwanza ulishirikiana na chama cha ODM kupitia kubuni serikali jumuishi, hatua iliyoleta udhabiti na maendeleo ya nchi,” alisema Mudavadi.
Aliysema hayo katika eneo la Butula, kaunti ya Busia, alipowahutubia wanachama 5,000 wa UDA, lengo la mkutano huo likiwa kuimarisha chama hicho mashinani.
“Mikutano ya mashinani inapaswa kufanikisha maendeleo na kutoa fursa bora kwa wananchi,” alisema Mudavadi.