Njuri Ncheke wamuidhinisha Naibu Rais Kithure Kindiki

Kulingana na baraza hilo, uongozi wa Rais Ruto na Kindiki utaimarisha  amani, udhabiti na maendeleo katika kaunti za Meru, Tharaka Nithi na taifa nzima kwa jumla.

Tom Mathinji
1 Min Read
Njuri Ncheke wamuidhinisha Naibu Rais Kithure Kindiki.

Baraza la Jamii ya Meru Njuri Ncheke, limemuidhinisha rasmi Naibu Rais Kithure Kindiki kuendelea na wajibu wake serikalini.

Aidha, Baraza hilo pia limetangaza kumuunga mkono Rais Willam Ruto kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027, liktoa wito kwa jamii ya Mlima Kenya kukumbatia umoja kabla ya uchaguzi huo.

Tangazo hilo lilitolewa katika mnara wa Nchiru, kaunt ya Meru ambako wazee hao pia walipnga juhudi zozote za kugawanya kura za mlima Kenya.

Akisoma taarifa ya baraza hilo, aliyekuwa Gavana wa Meru Kiraitu Murungi, alisema wazee hao wanamtambua Prof. Kindiki kama mwana wa Meru, huku wakimshukuru Ras William Ruto kwa kumteua kuwa Naibu Rais.

“Njuri Ncheke inawahimiza jami ya Ameru kusimama kidete na mwana wetu Kithure Kindiki, na kumuunga mkono Rais William Samoei Ruto,” ilisema taarifa ya baraza hilo.

Kulingana na baraza hilo, uongozi wa Rais Ruto na Kindiki utaimarisha  amani, udhabiti na maendeleo katika kaunti za Meru, Tharaka Nithi na taifa nzima kwa jumla.

Share This Article