Wakenya wahimizwa kujitenga na siasa za migawanyiko

Kulingana na waziri huyo, wananchi hawapaswi kukubali kutenganishwa na siasa, akisistiza kuwa viongozi wanajukumu kubwa la kuwaunganisha wakenya kwa ustawi wa taifa hili.

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku.

Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku, amewahimiza Wakenya kujitenga na siasa za migawanyiko, huku akiwataka kudumisha umoja taifa hili linapojiandaa kwa Uchaguzi Mkuu ujao.

Akizungumza alipohudhuria ibada ya Jumapili katika kanisa Katoliki la St. Joseph’s kaunti ya Meru, Ruku aliwahimiza wananchi kushirikiana na kuunga mkono serikali inapojizatiti kutekeleza maendeleo katika sehemu zote za nchi.

“Niliwahimiza wakazi wa kaunti ya Meru kushirikiana na kuunga mkono serikali ya Rais Willian Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua, wanapohudumia taifa hili,” alisema Ruku kwenye ukurasa wake wa X.

Kulingana na waziri huyo, wananchi hawapaswi kukubali kutenganishwa na siasa, akisistiza kuwa viongozi wanajukumu kubwa la kuwaunganisha wakenya kwa ustawi wa taifa hili.

Ruku alipigia debe tangamano wa kitaifa Kenya inapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2027.

TAGGED:
Share This Article