Shule za upili za Kakamega,Yala ya eneo la Nyaza na Highway ( Nairobi) leo jumapili zilianza kwa kishindo mashindano ya kitaifa ya muhula wa pili baina ya shule upili kwenye shule ya M – Pesa foundation mjini Thika.
Katika kundi A, Highway iliilaza Tononoka ya Pwani bao moja kwa nunge wakati Yala ikiiilemea Menengai ya Bonde la Ufa Magoli mawili kwa yai, kwenye kundi B, mabingwa mara 12 wa taji hilo Kakamega waliwazaba Tabaka ( kaskazini Mashariki) mabao matatu kwa nunge yaliyotingwa katika kipindi cha kwanza.
kesho jumatatu usubuhi, kakamega watakabana koo na Tumaini nao Tabaka wamalize udhia na Mwenda Andu. Saa nane, Menengai watachuana na Tononoka wakati Yala wakitifua kivumbi dhidi ya Highway.