Takriban wahamiaji 34 wamekufa maji wakijaribu kuingia Uhispania kutoka Morocco, kwa mujibu wa kiongozi wa eneo la Ceuta Jesús Vivas.
Kulingana na Vivas, wahamiaji wasiopungua 60,000 wamewasili katika eneo la Ceuta,Kaskazini mwa Uhsipania kutoka Morocco katika muda wa saa 24 zilizopita.
Vivas amesema idadi hiyo kubwa ya wahamiaji inaendelea kuwa mzigo kwa mji huo, ambao wakazi wake wanakisiwa kuwa takriban 83,000.
Wimbi hilo la wahamiaji linafwatia uamuzi wa mahakama ya upeo nchini Uhispania kwamba wahamiaji wanaozuiliwa baharini hawawezi kurejeshwa moja kwa moja nchini Morocco.
Waziri mkuu wa Uhispania Pedro Sánchez hata hivyo ametofuatiana na uamuzi huo, akisema wahamiaji wote haramu watarejeshwa nyumbani hivi karibuni.
Viongozi kadhaa wa Ulaya pia wameeleza wasiwasi wao, huku baadhi wakiahidi kuimarisha ulinzi wa mipaka.