Miili 6 yapatikana baada ya mashua kuzama Nigeria

Kulingana na mamlaka, mashua hiyo ilikuwa imewabeba wakulima na wafanyakazi waliokuwa wakirejea nyumbani kutoka shambani.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mashua yazama kaskazini mwa Nigeria.

Watu sita wamethibitishwa kufariki baada ya ajali ya mashua katika  mkoa wa Jigawa nchini Nigeria siku ya Jumapili.

Kulingana na mamlaka, mashua hiyo ilikuwa imewabeba wakulima na wafanyakazi waliokuwa wakirejea nyumbani kutoka shambani, duru zikiarifu kwamba ilikuwa na zaidi ya abiria 40 ajali hiyo ilipotokea.

Operesheni kubwa ya utafutaji na uokoaji inaendelea katika jamii wa Malamawar Yan Dutse, eneo la Ringim Lawan kufuatia ajali hiyo iliyotokea jumapili jioni.

Miili hiyo ilipatikana kutokana na juhudi za wapiga mbizi wanaoshirikiana na mamlaka kwenye operesheni hiyo.

Ajali za boti zinatokea mara kwa mara nchini Nigeria na mara nyingi zinatokana na kubeba mizigo kupita uwezo na hali mbaya ya hewa pamoja na hitilafu za uendeshaji.

TAGGED:
Share This Article