Sakaja akanusha kuongeza ada ya uegeshaji magari

Hata hivyo, wenye magari hawatatozwa ada ya kuegesha magari siku za Jumamosi na Jumapili.

Dismas Otuke
1 Min Read

Gavana wa jimbo la Nairobi Johnson Sakaja amepuuzilia mbali uvumi kuwa ada ya kuegesha magari imeongezwa.

Sakaja amewahakikishia wenye magari kuwa ada itasalia ilivyokuwa awali na kuwataka wenye magari kuchukulia taarifa hizo kuwa porojo.

Ameongeza kuwa ada ya maegesho ya magari itasalia shilingi 300 kwa siku au shilingi 5,000 kwa mwezi mmoja kwa magari madogo.

Magari aina ya Vans na Pick – Ups yatatozwa shilingi 500 kwa siku huku malori na mabasi madogo yakitozwa ada ya shilingi 1,000 kwa siku ama shilingi 12,500 kwa mwezi.

Hata hivyo, wenye magari hawatatozwa ada ya kuegesha magari siku za Jumamosi na Jumapili.

Share This Article