Aliyekuwa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp yamkini amekubali kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ujerumani.
Klopp, ambaye kwa sasa hana kazi, anatarajiwa kutia saini rasmi mkataba wiki ijayo baada ya pande zote kuafikiana nchini Marekani, wakati wa fainali za Kombe la Dunia.
Ujerumani haijakuwa na kocha tangu kujiuzulu kwa Julian Nagelsman mwezi Juni kutokana na matokeo duni ya ya timu katika Kombe la Dunia walipobanduliwa nje na Paraguay katika awamu ya 32.