Jorge Jesus ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Ureno, kutwaa nafasi ya Roberto Martinez aliyeng’atuka baada ya timu hiyo kubanduliwa na Uhispania kwenye Kombe la Dunia mwaka huu.
Shirikisho la Soka nchini Ureno limetangaza uteuzi wa Jesus baada ya kufunza vlabu kadhaa kwa zaidi ya miongo mitatu.
Hadi uteuzi wake, Jesus aliye na umri wa miaka 71, amekuwa kocha wa klabu ya Al -Nassr akiiongoza kunyakua taji la ligi kuu nchini Saudi Arabia baada ya miaka saba.
Akiwa Al-Nassr, Jesus amekuwa na nahodha Cristiano Ronaldo na mshambulizi Joao Felix .