Khamenei azikwa katika maabadi takatifu zaidi ya Iran

Shughuli rasmi za mazishi ya umma zilianza Jumamosi iliyopita.

Marion Bosire
2 Min Read

Mwili wa kiongozi mkuu aliyeuawa wa Iran Ali Khamenei, umezikwa kwenye maabadi takatifu zaidi ya Wa-Shia, miezi minne baada yake kuuawa kwenye mashambulizi ya angani dhidi ya makazi yake ya Tehran.

Vyombo vya habari vya serikali viliripoti mapema Ijumaa kwamba alikuwa amezikwa katika mji alikozaliwa wa Mashhad, ndani ya Madhabahu ya Imam Reza, jengo kubwa la kidini lenye kuba kubwa ya dhahabu na minara iliyopambwa kwa dhahabu katikati ya jiji hilo.

Sherehe ya mazishi ilifanyika kwa faragha, baada ya wiki moja ya maombolezo ya umma na maandamano yaliyovutia umati mkubwa unaokadiriwa kufikia zaidi ya watu milioni 15 na huenda ukawa zaidi ya mara mbili ya idadi hiyo kulingana na makadirio ya Iran.

Hata hivyo Mojtaba Khamenei, mwana wa Khamenei na mrithi wake kama Kiongozi Mkuu wa Iran, hakuhudhuria shughuli za mazishi.

Hajaonekana hadharani tangu shambulio la Februari 28 ambalo, kwa mujibu wa taarifa hiyo, lilimuua baba yake na kuashiria mwanzo wa vita vya Marekani ikishirikiana na Israel dhidi ya Iran.

Mazishi ya Khamenei yalikuwa yamepangwa kufanyika mwezi Machi, lakini yakaahirishwa baada ya Iran kutumbukia vitani.

Shughuli rasmi za mazishi ya umma zilianza Jumamosi iliyopita wakati maelfu ya raia wa Iran walikusanyika katika jengo la kidini la Grand Mosalla mjini Tehran, ambako jeneza la Khamenei liliwekwa ili wananchi watoe heshima zao za mwisho.

Wajumbe kutoka makundi washirika wa Iran katika eneo hilo, yakiwemo Hamas na Islamic Jihad kutoka Gaza, Hezbollah kutoka Lebanon na Wahouthi kutoka Yemen, walihudhuria.

Share This Article